BODI YA USHAURI YA MNMRRH-MUSOMA YAFANYA ZIARA DODOMA-RRH

Posted on: September 29th, 2026

Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere - Musoma leo imefanya ziara ya mafunzo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma.

Lengo la ziara hiyo ni kujifunza mifumo bora ya utoaji wa huduma za afya na usimamizi wa hospitali, ili kwenda kufanya maboresho katika Hospitali ya Musoma.

Katika ziara hiyo wajumbe wametembelea Idara ya Wagonjwa wa Dharura, Maabara Kuu, Wodi za Wazazi na kujionea mfumo wa kidijitali wa kuhudumia wagonjwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Musoma amesema wamefika Dodoma kujifunza yale mazuri yanayofanyika ili kwenda kuboresha huduma za afya Musoma.

Kwa Upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma Dkt. Ibenzi Ernest amesema wapo tayari kushirikiana na Musoma katika kubadilishana uzoefu kwa ajili ya kuboresha afya ya Mwananchi

Ziara hiyo imehitimishwa kwa kikao cha pamoja cha kubadilishana uzoefu.