KAMBI MAALUMU MATIBABU YA MIFUPA KUFANYIKA DODOMA-RRH
Posted on: September 26th, 2026Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma inawaalika wananchi wenye changamoto za mifupa kujitokeza kupata huduma za kibingwa na upasuaji, katika kambi maalum ya huduma za mifupa inayofanyika mkoani Dodoma.
Kambi hiyo inafanyika kuanzia Septemba 28- 30, 2026, ambapo madaktari bingwa wa mifupa watatoa huduma za uchunguzi, matibabu pamoja na upasuaji kwa wagonjwa watakaohitaji huduma hiyo.
Aidha, Kambi hiyo imeandaliwa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Madaktari wa Mifupa Tanzania (TOA) unaotarajiwa kufanyika Oktoba 1- 3, 2026, jijini Dodoma.
Mbali na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma, huduma hizo pia zinatolewa katika hospitali za DCMC, UHURU na St. GEMA.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma,inatoa fursa kwa wananchi kupata huduma hiyo ya kambi ya matibabu ya mifupa.



