KUIMARISHA UJUZI, KUBORESHA HUDUMA
Posted on: September 13th, 2026Baadhi ya Madaktari bingwa wa magonjwa ya mifupa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma, kwa kushirikiana na wadau pamoja na madaktari kutoka taasisi mbalimbali, wameendelea kutoa mafunzo kwa wataalam wa afya kuhusu namna bora ya kutibu na kuhudumia wagonjwa wenye changamoto za mifupa ndani na nje ya Mkoa wa Dodoma.
Wataalam hao walifanya mafunzo maalumu mkoani Mbeya, yaliyolenga kuongeza ujuzi na uwezo wa wataalam wa afya katika utoaji wa huduma za matibabu ya mifupa kwa njia mbalimbali. kuanzia Septemba 14 - 17,2026.
Aidha, Miongoni mwa mada na vitendo vilivyofundishwa ni pamoja na namna sahihi ya kufunga P.O.P (Plaster of Paris) kwa wagonjwa wenye matatizo ya mifupa, pamoja na mbinu nyingine za msingi katika matibabu na huduma za mifupa. Mafunzo hayo yalihusisha wataalam wa afya kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Mbeya, ambapo walipata fursa ya kujifunza kwa nadharia na vitendo kutoka kwa madaktari bingwa na wataalam wenye uzoefu katika eneo hilo.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma inaendelea kushirikiana na taasisi na wadau mbalimbali katika kubadilishana uzoefu na maarifa ya kitaalam, kwa lengo la kuimarisha huduma za afya na kuwafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.



