MBUNGE WA DODOMA MJINI AFANYA ZIARA DODOMA-RRH

Posted on: July 13th, 2026

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mhe. Paschal Inyasi Chinyele amefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kujionea huduma zinazotolewa na changamoto zinazowakabili wagonjwa.

Akizungumza na Afisa Mawasiliano na uhusiano kwa umma wa Hospitali hiyo Julai 14, 2026 mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma. amesema ziara hiyo ni sehemu ya wajibu wake wa kibunge wa kusimamia utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wa jimbo lake la Dodoma Mjini.

Chinyele amesema amefurahishwa na juhudi za uongozi wa Hospitali katika kuboresha huduma zinazotolewa na kwamba kupitia ofisi yake anaahidi ushirikiano .

"Wananchi wa Dodoma Mjini wanastahili kupata huduma bora. Nimeona kuna kazi nzuri inafanyika hapa na kwa hakika nawapongeza sana viongozi na watumishi kwa kazi kubwa wanazozifanya.
amesema Chinyele.

Aidha, amesema kuwa huduma zinazotolewa Hospitalini hapo ni nzuri kwani wagonjwa aliozungumza nao wamekiri kuridhishwa na Huduma wanazozipata.