UWT WILAYA YAWAGUSA WAHITAJI
Posted on: September 29th, 2026Septemba 30, 2026
Ikiwa ni wiki ya Maadhimisho ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), iliyoanza Septemba 28 na kilele cha maadhimisho hayo ikiwa ni Octoba 4, 2026. Umoja wa wanawake Tanzania Wilaya ya Dodoma Mjini wamefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma kwa ajili ya kufanya Matendo ya huruma, Lengo ikiwa ni Kuwagusa wahitaji waliopo Hospitalini hapo.
Mwenyekiti wa UWT Bi. Zabibu Juma Mtoro amesema wamefika Hospitali kuunga Mkono utoaji wa Huduma ndani ya hospitali kwani miongoni mwa wanao hudumiwa ni wagonjwa wenye uhitaji .
“Sisi kama UWT wilaya ya Dodoma Mjini tumekuja Hapa kwa lengo la kuwagusa wahitaji ikiwa ni ishara ya upendo” Amesema Bi. Zabibu
Akizungumza mara baada ya kuwakaribisha na kuwapokea wageni hao, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma, Dkt. Ibenzi Ernest amewashukuru na kuwapongeza UWT wilaya kwa kufika na kutoa mchango wao kwa wahitaji.
“Asanteni sana kwa kuja tunawashukuru kwa kuendelea kuunga Mkono juhudi za utoaji wa Huduma kwa watanzania wenzetu” amesema Dkt. Ibenzi



