KINYWA NA MENO

IDARA YA KINYWA NA MENO
Historia fupi

Idara ya Meno ya hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ni moja ya idara kongwe ikiwa ilianzishwa miaka ya 1960. Waanzilishi walikuwa ni Dr Helmut ,Dr. Mmari, Dr Mgalula, dr Kelvin. Mr Manyata, Mr Ruta, Ms Lea.

Wakuu wa idara toka wa kwanza paka aliyepo sasa ni kama ifuatavyo; Dr Helmutt (mjerumani) ndiyo alikuwa wa kwanza, akafuata Dr Mmari, Dr Kelvin, Dr Nyerere, Dr Kalyanyama, Dr Kidyala, Dr Chembele, Dr Seseja, Dr Mrosso, Dr Masele (ndo aliyepo sasa).
Huduma zitolewazo
Idara ya kinywa na meno inatoa mbalimbali nyingi ambazo zimegawanyika katika sehemu tatu
1. Upasuaji
2. Uzibaji meno
3. Meno bandia


1. Upasuaji
Huduma hii inahusu upasuaji mkubwa, upasuaji mdogo na kung’oa meno. Upasuaji mkubwa hufanyika kuondoa mavimbe makubwa yanayotokea eneo la kinywa, mataya na usoni. Mavimbe hayo yanaweza kuwa ya kansa, yasiyo ya kansa au vifuko vilivyojaa maji(cysts). Upasuaji mkubwa pia hufanyika kuunganisha mifupa ya usoni na mataya kwa wagonjwa waliopata ajali.
Upasuaji mdogo hufanyika kwa ajili ya kuondoa vivimbe vidogo au majipu ya eneo la kinywa na meno, na hufanyika kama matibu au kuchukua kipimo kwa ajil ya uchunguzi zaidi(biopsy).
Ung’oaji meno hufanyika kwa meno ambayo yametoboka sana na hayawezi kuzibika, pia meno ambayo yameathirika na ugonjwa fizi au ajali.

2. Uzibaji meno
Huduma hii inapatikana katika idara yetu pia, inahusisha kuziba jino ambalo limetoboka. Kama jino limetoboka kiasi tunaziba kwa dawa ya kudumu moja kwa moja (permanent filling), au tunaweza kuweka dawa ya kulifanya jino kujijenga (pulp capping +temporary filling) na hapa utaambiwa urudi baada ya wiki sita kuja kumalizia matibabu. Kwa meno ambayo yametoboka sana huwa yanafanyiwa tiba ya mzizi(root canal treatment) ambapo mgonjwa atawekewa ganzi kisha jino kusafishwa paka kwenye kiini chake, baada hapo litazibwa kwa dawa ya muda mfupi na mgojwa ataambiwa arudi baada wiki moja kwa ajili ya kumalizia tiba.

3. Meno bandia
Huduma hii pia inapatikana katika idara yetu, meno tunatengeneza ni ya kuweka na kutoa(removable dentures) iwe mdomo mzima(full) au baadhi tu ya meno(partial), pia tunatengeneza meno bandia ambayo sio ya kutoa, pia tiba ya kupangilia meno yaliyojipanga vibaya inafanyika kwa vifaa maalum vya kuvaa na kuvua(removable orthodontic appliances).
Kwahiyo wananchi wote wanakaribishwa kupata huduma katika idara yetu na tumejipanga kuwahudumia.
Kwa ufafanuzi zaidi, mawasiliano yetu ni
Dr Athanase Masele, mkuu wa idara , mobile 0717201265 email; amasele@gmail.com
Sr Martha Masimba ,nurse incharge wa idara, mobile 0715880048