WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITAL YA RUFAA YA MKOA DODOMA

Posted on: November 15th, 2025

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba leo Novemba 15, 2025 amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, na kuziagiza Hospitali zote nchini zihakikishe ,wajawazito wanapofika hospitali wahudumiwe kwa haraka, ili kuokoa maisha ya mama na mtoto.


Waziri Mkuu pia ameiagiza Wizara ya Afya, Bohari ya Dawa (MSD) na Hospitali zote nchini, Kuweka vipaumbele vya kuwa na dawa kulingana na mahitaji ya eneo husika. “ Haipendezi mwananchi kufika hospitali na kupatiwa vipimo vyote kisha anaambiwa dawa akanunue kwingine, kama duka binafsi linaweza kupata dawa hizo, inawezekanaje hospitali za serikali hapati? Naagiza Hospitali zote ziwe na dawa.”


Ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wananchi nje ya hospitali , baada ya kutembelea wananchi waliofika hospitalini hapo .