MAADHIMISHO KUELEKEA MIAKA 60 YA UHURU

Posted on: December 5th, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameongoza watanzania katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika tarehe 09 Desemba, 2021katika  uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam

Katika Sherehe hizo, Mhe. Rais Samia amekagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi na usalama na kupokea  salamu za utii, kisha gwaride hilo kupita kwa heshima mbele yake kwa mwendo wa pole na mwendo wa haraka.

Sherehe za maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru zimehudhuriwa na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye alikuwa mgeni rasmi, Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame, Rais wa Msumbiji Mhe. Philepe Nyusi, Rais wa Visiwa vya Comoro Mhe. Azali Assoumani, wawakilishi wa Viongozi kutoka nchi za Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Oman na Uswatini pamoja na Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Wakati huo huo, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametunuku Nishani 14 ikiwa ni sehemu ya Nishani 893 alizozitunuku kwa Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama nchini.