TUMEJIPANGA VYEMA KUTOA HUDUMA BORA NA KWA WAKATI

Posted on: February 29th, 2024

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma Dkt. Ibenzi Ernest ambaye pia ni Mwenyekiti wa Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa, amesema Hospitali za Rufaa zimejipanga vyema kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi , na hii ni kufuatia baadhi ya Hospitali kusitisha huduma kwa wanachama wa Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya.(NHIF)

Ameyasema hayo Machi 01,2024 wakati akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dodoma kuhusu namna Hospitali za Rufaa zilivyojipanga katika kuwahudumia Watanzania.

"Kwa sasa tumeongeza muda wa kutoa huduma, tunao wataalamu wa kutosha , na tumejipanga vyema katika kutoa huduma kwa muda wote" amesema Dkt. Ibenzi.