VIONGOZI BODABODA WAPEWA SEMINA

Posted on: March 27th, 2024

Jijini Dodoma.
Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma kupitia Idara ya Magonjwa ya Dharura na nje, wamefanya semina elekezi kwa viongozi wa Maafisa usafirishaji ( bodaboda )
Lengo kuu ikiwa kuwajengea uwezo wa namna nzuri ya kuokoa manusura wa ajali, kutoa huduma ya kwanza pindi ajali ikitokea pamoja na elimu kuhusu aina za majeraha na namna ya kupunguza madhara zaidi yatokanayo na ajali mbalimbali.

Hospitali pia inaendelea na mpango uitwao " OKOA MAISHA" Ambapo watumishi wa hospitali wanatarajia kukutana na maafisa usafirishaji (bodaboda) katika vituo mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu .