Homa ya Manjano

Posted on: July 13th, 2024
Kituo cha kutolea chanjo ya Homa ya Manjano(Yellow Fever) Kituo kilianza tarehe 12/Mar/2019 Kituo hiki kilianzishwa baada ya kuona kuna uhitaji mkubwa kwa jamii kuhusu huduma hii, pia baada ya Serikali kuhamia hapa Dodoma.Huduma ya chanjo ya Homa ya Manjano inatolewa kwa Tsh 30,000/= tu Chanjo hii inatolewa kwa wasafiri wanaoenda nje ya Nchi.Chanjo hii ni salama na hutolewa Mara moja tu kwa maisha.Chanjo hii hutolewa kila Jumatano ya wiki, endapo itatokea wateja wanao fikia 10 chanjo hii inaweza tolewa siku yyte katika wiki.Chanjo hii haipo kwenye Bima wala msamaha.Kwa watoto chini ya miaka 2, wenye magonjwa ya muda mrefu, wazee zaidi ya miaka 60, na wenye mzio na mayai hao hawatapa chanjo ya Homa ya Manjano (Exempted) badala yake watalipia Tsh 10,000/= tu na kupatia "Kadi ya Exemption".Karibuni kwa huduma bora kabisa ya Chanjo ya Homa ya Manjano, karibu tukuhudumie.
Contact Person
Richard Lupeja
0758528566
0713888765