Public Health Education

Homa ya Manjano
Saratani ya Shingo ya Kizazi

SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI NI NINI?

Saratani ya shingo ya kizazi ni saratani ambayo hutokana na mabadiliko ya mfumo wa chembechembe au cells zilizoko katika shingo ya kizazi. Mabadiliko haya hupelekea chembe chembe hizo kushamiri na kuzaliana kwa kasi kinyume na mpangilio wa maumbile.Saratani ya Shingo ya kizazi yasemekana kuwa ni saratani inayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanawake katika nchi zinazoendelea. Ripoti ya 2012 ya shirika la afya duniani 'WHO' imesema kati ya matukio 75,000 ya waathirika wa saratani ya kizazi barani Afrika, 50,000 walifariki dunia.

NINI KINACHOSABISHA SARATANI YA SHINGO YA UZAZI?

Ripoti za utafiti wa kisayansi zimeafiki kuwa asilimia 99% ya saratani za shingo ya kizazi hutokana na maambukizi ya virusi vya 'Human Papillomavirus' au HPV vilivyoko katika jamii ya papilloma. Baadhi ya virusi hivi vyenye aina zaidi ya mia moja huambukizwa kwa njia ya kujamiana.

BAADHI YA MAMBO YANAYOONGEZA HATARI ZA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Kushiriki tendo ndoa katika umri mdogo au chini ya miaka 18.

Kuwa na wenzi tofauti au mwenzi aliye na wapenzi tofauti.

Utumiaji wa sigara kwani hupunguza nguvu ya kinga mwilini(impairs immune system).

Watu wenye kinga hafifu ya mwili au magojwa kama Ukimwi.

Uzazi wa mara kwa mara

BAADHI YA DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Kutokwa na majimaji au uchafu wenye harufu kali ukeni.

Kutokwa na damu ukeni mbali na siku za mwezi au baada ya tendo la ndoa.

Maumivu makali ya sehemu ya chini ya tumbo ( pelvic area).

Kuhisi maumivu makali wakati wa kujamiiana.

Kupungua kwa uzito wa mwili bila kukusudia.

Mkojo wenye matone ya damu

JE SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI HUTIBIKA?

Saratani ya shingo ya kizazi yaweza kutibika iwapo itagundulika mapema. PAP TEST (PAPANICOLAOUS TEST);Pap-Smear ni kipimo ambacho hutumika kuchunguza mabadiliko ya chembe zilizoko katika mlango wa kizazi ili kugundua mabadiliko yanayotokea katika chembe hizo na hivyo kuwahi kuyakabili mapema.

UMRI WA KUPATA PAP TEST

Test hii hushauriwa kwa wanamke wa umri wa miaka 21 hadi 65 na chini ya umri wa miaka 21 endapo ameingia katika tendo la ndoa kwa kipindi kisichopungua miaka 3.

KUPUNGUZA HATARI ZASARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Pap tests.

Waweza kupata Pap test mara 1 kwa mwaka au mara 1 kwa miaka 2- 3,hii itategemea ushauri wa daktari,umri,hali yako ya afya kwa ujumla, na majibu uliyoyapata katika testi zilizotangulia na mfumo wako wa maisha.

Pata HPV vaccine (hii yashauriwa kati ya umri wa miaka 12 hadi 26 chini ya mwongozo wa daktari) .

Kuwa na mpenzi mmoja.

Mahusiano ya kimwili na mtu mmoja hupunguza hatari za maambukizi ya magojwa ya zinaa.

Tumia kinga . 

Hii husaidia kupunguza maambukizi ya magojwa ya zinaa.


read more
Mafunzo ya eHMS

Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kupitia Kitengo cha TEHAMA inaendelea kutoa mafunzo watumishi wake jinsi ya kutumia mfumo wa eHMS kukusanya, kutunza na kutumia taarifa za wagonjwa

read more